Wimbi La Siasa

Informações:

Sinopsis

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Episodios

  • Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi yaanza mazungumzo jijini Nairobi

    10/05/2024 Duración: 10min

    Mazungumzo ya amani yanayohusisha makundi ya waasi nchini Sudan Kusini na serikali yameanza rasmi jijini Nairobi, wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwezi Disemba. Makundi haya ni yale yaliosusia mkataba wa amani wa mwaka 2018, wakati rais Salva Kiiri na hasimu wa wake wa kisiasa ambaye sasa ni makamo rais wa Kwanza Reik Machar walisaini mkataba wa amani.Soma piaKenya kuisaidia Sudan Kusini kupata suluhu ya utovu wa usalama wa miaka mingiKatika makala haya Benson Wakoli na wachambuzi wa kisiasa Fracis Wambete, ambaye na mhadhiri wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, pamoja na Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka nchini Tanzania wanajaribu kuangazia kufaulu kwa mazungumzo haya, skiza.

  • Nini haki za wafanyakazi duniani ?

    01/05/2024 Duración: 10min

    Kila tarehe 1, ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani. Wafanyakazi wanatumia siku hii kusherehekea mafanikio yao na kuendeleza mapambano ya haki zao. Je, siku hii ina umuhimu gani ? Wageni wetu ni Nice Mwansasu kutoka  Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na mwanasheria wa masuala ya ajira kutoka Kenya Elvis Abenga

  • Mwaka mmoja wa mapigano nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na RSF

    17/04/2024 Duración: 09min

    Wiki hii, ilikuwa ni mwaka mmoja wa vita nchini Sudan, kati ya jeshi la taifa chini ya Jenerali  Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF wanaongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo. Mwaka mmoja baadaye, vita vimeendelea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, huku wengine Milioni 8.5 wakiyakimbia makaazi yao wakiwemo Milioni 1.8 waliokwenda kutafuta hifadhi katika nchi jirani kama Chad.

  • Uhusiano kati ya Somalia na Ethiopia waendelea kuingia baridi

    10/04/2024 Duración: 09min

    Wiki iliyopita, Somalia ilimfukuza nchini mwake Balozi wa Ethiopia Mukhtar Mohamed kwa madai kuwa nchi hiyo inaingilia mambo yake ya ndani.Mwezi Januari, mzozo wa kidiplomasia ulianza kushuhudiwa nchini humo baada ya Ethiopia kuingia kwenye makubaliano na jimbo la Somaliland, kutafuta njia ya kufika baharini na kujenga kambi ya jeshi kwenye ukanda wake wa pwani.Nini hatima ya mvutano huu ?

  • Maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ,ulimwengu umejifunza nini?

    03/04/2024 Duración: 09min

    Kumbikizi ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu hadi laki 8 ,kuna wito wa ulimwengu kuhakikisha watuhumiwa zaidi kusakwa  na mataifa yaweke mikakati kuzuia mauaji kama haya kutojirudia Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, sasa linataka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya kuwasaka watuhumiwa zaidi wa mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda, ambapo mwishoni mwa juma hili, Kigali itafanya kumbukizi ya miaka 30.

  • Raia wa Senegal wamchagua Faye kuwa rais wao mpya

    27/03/2024 Duración: 10min

    Bassirou Diomaye Faye amechaguliwa kuwa rais mpya wa Senegal.Faye mwenye umri wa miaka 44, mshirika wa karibu wa mwanasiasa mwenye ushawishi Ousamane Sonko, ameahidi kufungua ukura mpya wa uongozi wa nchi hiyo.Kwanini raia wa Senegal wamemchagua Faye ? Tunachambua pamoja na Mali Ali akiwa jijini Paris, na Lutege Musa Lutege akiwa jijini Dar es salaam.

  • Burundi: Mgawanyiko kwenye chama kikuu cha upinzani  CNL

    13/03/2024 Duración: 10min

    Nchini Burundi, chama kikuu cha upinzani cha CNL kinashuhudia mgawanyiko baada ya kiongozi wake Agathon Rwasa kuondolewa kwenye nafasi kiongozi wa chama.Hii ilitokea wakati Rwasa akiwa ziarani nchini Kenya.Nini hatima ya kisiasa ya Rwasa  ?Tunazungumza naye lakini pia Mali Ali mchambuzi wa siasa za Burundi akiwa jijini Paris.

  • Kenya: Kutuma polisi wake nchini Haiti kuthibiti magenge ya wahalifu

    08/03/2024 Duración: 09min

    Serikali ya Kenya na Haiti zimetiliana  saini ili kufanikisha Kenya kutuma polisi wake nchini Haiti kudhibiti magenge ya wahalifu ambayo yameendelea kutatiza usalama nchini Haiti. Katika makala haya Domic Wabala mchambuzi wa usalama na dkt Braine Wanyama, mchambuzi wa siasa za kimataifa wanatathimini nini maana ya Kenya kutuma polisi kule Haiti.

  • Uongozi wa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika jumuiya ya Afrika Mashariki

    28/02/2024 Duración: 10min

    Rais Salva Kiir amekuwa ziarani Rwanda na Burundi kuangazia swala la usalama

  • AU yakosa kupata suluhu kwa mizozo ya Africa

    21/02/2024 Duración: 10min

    Viongozi wa Africa wamekutana mwisho wa juma katika mkutano wao wa kila mwaka wa 37, nchini Ethiopia walishindwa kuja na njia ya mapoja kumaliza migogoro barani. Je tatizo la Africa nini?Je Africa inaweza jitegemea? ndio baadhi ya maswali Benson Wakoli, na wachmbuzi mwanadiplomasia Macharia Munene pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa dkt Braine Wanyama wanajaribu kuyajibu katika makala haya.

  • Wabunge nchini Tanzania wapitisha mageuzi ya sheria za uchaguzi

    07/02/2024 Duración: 09min

    Wiki iliyopita, wabunge nchini Tanzania, walipitisha miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. Tume ya uchaguzi itabadilishwa jina na sasa itafahamika kama Tume huru ya taifa ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake, watateuliwa na rais baada ya kupokea majina matatu kutoka kwenye Kamati ya usaili.Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kinapinga mabadiliko hayo.  Wachambuzi wetu ni Mohammed Jawadu akiwa Dar es salaam  na Hamdun Marcel akiwa Mwanza.

  • Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS

    03/02/2024 Duración: 09min

    Mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso, yametangaza kujiondoa kwenye muungano wa ECOWAS, baada ya vikwazo ambayo muungano huu ulitangaza dhidi ya mataifa hayo, kipindi baada ya mapinduzi ya kijeshi. Benson Wakoli pamoja na wachanganuzi wa siasa za kimataifa, dkt Braine Wanyama na Mali Ali, wanatathimini Athari ya Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS.Skiza makala haya.

  • Matarajio ya wakongo baada ya kuapishwa kwa rais Félix Tshisekedi

    24/01/2024 Duración: 10min

    Wimbi la siasa imeangazia fursa iliyopo kidiplomasia kwa rais wa DRC Felix Thisekedi aliyeapishwa Jumamosi iliyopita, kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili.DR Congo, imekuwa kwenye mvutano wa kidiplomasia na Rwanda, kwa madai kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 eneo la mashariki. Ruben Lukumbuka amewaalika Francois Alwende, mtaalamu wa siasa za DRC akiwa jijini Nairobi pia  Guerschome Kahebe pia ni mchambuzi wa siasa akiwa Jijini Washington nchini Marekani.

  • Mvutano kati ya ofisi ya rais nchini Kenya na idara ya mahakama

    17/01/2024 Duración: 10min

    Rais wa Kenya William Ruto, ameingia kwenye mvutano na idara ya Mahakama. Ruto anasema Mahakama imejawa na Majaji mafisadi, wanaopindisha haki na kukwamisha miradi za serikali. Jaji Mkuu Martha Koome amekanusha madai hayo. Nini hatima ya mvutano huu ?

  • Mkataba kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland, kizungumkuti

    10/01/2024 Duración: 10min

    Makala hii imejadili hatua ya rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kusaini sheria ya kufuta makubaliano kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland, hii ikiashiria kutoridhishwa na matumizi ya bandari ya Berbera, uamuzi unaoibua hofu ya kutokea mgogoro baina ya pande hizo mbili.Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameangazia hili pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Washington Marekani, Abdullahi Boru pamoja na profesa Macharia Munene ni mchambuzi wa siasa, na mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia akiwa Jijini Nairobi hapa Kenya

  • Utendakazi wa CENI na mrengo wa upinzani katika uchaguzi wa Disemba 20

    05/01/2024 Duración: 10min

    Maandamano yaliotishwa na upinzani kupinga utendakazi wa CENI yalizimwa na polisi nchini DRC

  • Raia wa DRC wapiga kura kumchagua rais na viongozi wengine

    23/12/2023 Duración: 08min

    Wananchi wa DRC zaidi ya Milioni 40 wanapiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani. Tunachambua kwa kina.

  • Ripoti ya kamati ya maridhiano nchini Kenya

    30/11/2023 Duración: 09min

    Suala la gharama ya maisha kupunguzwa lilikosa kupewa nafasi kwenye vikao vya jopo la maridhiano

página 1 de 2